KARELIS AMSUGULISHA BENCHI SAMATTA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta mambo yanaonekana kuwa si mazuri sana kwa upande wake kadiri siku zinavyokwenda mbele, kwa nini?Uwepo wa Nikolaos Karelis ni kigingi kwa Samatta kupata fursa ya kuonesha uwezo kwake katika timu anayoichezea Ubelgiji KRC Genk.
Samatta ametokea benchi kwenye mechi zote alizocheza hadi sasa kuchukua nafasi ya mshambuliaji raia wa ugiriki Karelis Nikolous. Lakini katika mechi waliyoshinda 1-0 dhidi ya Genk Samatta alipewa muda mchache zaidi wa kucheza akiingia dakika ya 85 kuchukua nafasi ya Karelis, dakika chache hizo zilizobaki hazikumtosha Mtanzania huyo kufanya madhara yoyote.
Ushindi wa bao 1-0 iliopata KRC Genk dhidi ya Rapid Wien unaipa nafasi timu hiyo inayotumikiwa na Mbwana Samatta kufuzu moja kwa moja hatua ya mtoano ya Ligi ya Uropa msimu huu.
Comments
Post a Comment