AFRICA LYON YAVURUGA MIPANGO YA SIMBA SC, YANGA YATAKATA MBEYA

Tokeo la picha la africa lyon fc

Na HUSSEIN MKUWIA.

Ligi kuu tanzania bara imeendelea leo katika viwanja tofauti,huma macho na masikio ya wapenzi wengi wa soka wakielekeza jijini Daresalaam na kule jijini Mbeya.

Africa Lyon ilikuwa mwenyeji wa Simba katika uwanja wa uhuru jijini Daresalaam katika mchezo simba ilionekana ikiwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira kwa asilimia kubwa na kushambulia kwa kasi lango la Lyon na lyon ikonekana kujilinda zaidi kuliko kushambulia ndipo dakika 45 za kipindi cha kwanza zikamalizika pasipo mafanikio kwa timu zote.

Dakika 45 za kipindi cha pili zilianza kwa simba kupeleka mashambulizi kwenye lango la wapinzani wao lakini lyon walisimama imara na kuhakikisha washambuliaji wa simba hawapati nafasi ya kutumbukiza mpira nyavuni na ndipo lyon ilipofanikiwa kupeleka kilio kwa wanamsimbazi kupitia mshambuliaji wake Abdallah dakika za lala salama na kufanya mbao ya matangazo kusoma Lyon 1-0 Simba sc.

Wakati lyon wakipeleka kilio kwa wanasimba watani wao wa jadi Yanga sc wametakata baada ya kuwapigisha kwata maafande wa magereza kutoka jijini Mbeya goli 1-0 mchezo ulifanyika katika dimba la kumbukumbu ya sokoine jijini mbeya.


Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU