Posts

Showing posts from 2016

MOURINHO ABADILI MAWAZO YAKE KWA VICTOR LINDELOF

Image
BBC wamejipatia standard ya juu kwasababu mara nyingi huwa hawakosei juu ya ishu za usajili. Sasa hivi wameripoti kwamba Mourinho amebadirisha mawazo yake juu ya kumsajili mchezaji Victor Lindelof kutoka Benfica. Imeripotiwa sana kuhusu mchezaji huyu kuelekea kujiunga na club ya Manchester united ambapo alisaini hadi jezi ya Manchester ambayo alikuwa nayo shabiki mmoja. BBC wameandika kwamba Jose ameshawishiwa kwa uzuri wa Rojo na Jones kwenye ulinzi sehemu ya katikati kiasi cha kubadirisha maamuzi ya kutaka kumnunua mchezaji huyo. Jose pia ana imani kubwa na Eric Bailly, Chris Smalling na Daley Blind. Lindelof ilitoka taarifa kwamba zingetumiwa Euro millioni 45 ili awezeze kuhamia Manchester United kutoka Benfica, Kiasi hiki kingekua kikubwa zaidi kwa Benfica tangu waanze kuuza wachezaji.

FRANSIS CHEKA AKUTANA NA KIBANO CHA TPBC

Image
Jana December 30, 2016 Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC) imetangaza kumfungia kwa miaka miwili Bondia wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka kufuatia kitendo chake cha kugoma kupanda ulingoni kupigana na Bondia Abdallah Pazi “Dullah Mbabe”. Pambano hilo ilikuwa lifanyike Desemba 25 mwaka huu, katika Ukumbi wa PTA Saba saba jijini Dar es salaam, lililoandaliwa na Promota Siraju Kaike kupitia kampuni yake ya Kaike Promotion. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, Katibu Msaidizi wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC), Chatta Michael amesema kuwa Kamisheni yake ilitoa kibali cha kufanyika kwa mpambano huo baada ya kujiridhisha kuwa taratibu zote zimefuatwa na mabondia wameridhia na kukubaliana na muandaaji, Ila wameshangwaza na Bondia Francis Cheka kugoma kupanda ulingoni kwa madai ya malipo wakati alishasaini mkataba na muandaaji ulioonyesha kuwa ameshachukua kiasi cha shilingi mil...

RONALDO AKATAA PAUNI MILIONI 310,000 KWA WIKI

Image
Klabu ya Real Madrid ilipewa takriban pauni milioni 250 na klabu ya China ambayo haikutajwa jina ili kumnunua nyota wake Cristiano Ronaldo kulingana na ajenti wake Jorge Mendes.Amesema kuwa nahodha huyo wa Portugal mwenye umri wa miaka 31 hana haja na mpango huo ambao ulishirikisha mshahara wa kila mwaka wa pauni milioni 85. Ronaldo alisema kuwa anaweza kucheza kwa miaka mingine 10 mnamo mwezi Novemba baada ya kuandikisha mkataba mpya na Real Madrid hadi Juni 2021.''Soko la China ni soko jipya.wanaweza kuwanunua wachezaji wengi, lakini haiwezekani kumnunua Ronaldo'', alisema Mendes. ''Cristiano ndio mchezaji bora duniani, ni kawaida kupata maombi'', aliongezea raia huyo wa Ureno.Chini ya ombi hilo analodai Mendes, Ronaldo angepokea kitita cha pauni milioni 1.6 kwa wiki ikiwa ni mara tatu ya zaidi ya kitita cha uhamisho wa pauni milioni 89 zilizogharimu uhamisho wa Paul Pogba kutoka Juventus kuelekea Manchester United. Mendes aliambia Sky...

"SINA MPANGO NA SOKA LA CHINA" - ZLATAN IBRAHIMOVIC

Image
Mchezaji wa klabu ya Manchester United, Zlatan Ibrahimovic pamekuwa na taarifa zinasema kuwa amezikatalia klabu za nchini China, hizi ni zile klabu ambazo zimekuwa na nia ya kumsajili akakipige kule kwao. Uongozi wa Manchester United umejipanga kuzungumza na mchezaji huyo ambaye saivi anamagoli 12 katika ligi ya EPL ili kumuongezea mkataba mpya wa kuendelea kubakia United.

MWENYEKITI MPYA WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI AKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA H...

Image

WALIOFAULU DARASA LA SABA LAZIMA WAANZE ELIMU YA SEKONDARI

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitavumilia kuona mamia ya vijana waliofaulu mitihani ya darasa la saba na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza wanabaki nyumbani eti kwa kuwa hakuna madarasa ya kutosha. “Serikali haitaridhika kuona vijana waliofaulu vizuri wanashindwa kwenda kidato cha kwanza. Halmashauri zilijua tangu mapema ni wanafunzi wanaenda shule za msingi kwa hiyo inataka kuona wote waliofaulu wanakwenda sekondari kwa asilimia 100,” amesema. Ametoa kauli hiyo leo mchana wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa mkoa wa Lndi mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo kwenye Ikulu ndogo wilayani Nachingwea. Waziri Mkuu amewasili wilayani Nachingwea akiwa njiani kuelekea Ruangwa kwa mapunziko ya mwisho wa mwaka. Amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kutoa elimu ya bure kwa kila mtoto sasa iweje watoto wengine wanafaulu na wanashindwa kujiunga na elimu ya sekondari. “Tumesema elimu ni bure hakuna sababu ya kufanya wengine wasiende shule wakati ...

HAJI MANARA AMUOMBEA MSAMAHA JERRY MURO KWA RAIS WA TFF

Image
December 25 2016 mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Club ya  Simba   Haji Manara  alitumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe kwa Rais wa  TFF  Jamal Malinzi  kumuomba asamehewe afisa habari mwenzake wa  Yanga   Jerry Muro  ambaye amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka. Kwako Rais wa TFF Kwanza nikutakie heri na baraka ktk sikukuu hii kubwa kabisa duniani kote. Nnakuandikia ujumbe huu mfupi na wa wazi kwako, nikiamini wewe ni mtu mwelewa na mwenye huruma na upendo, pia ni kiongozi mwenye maono ya dhati kwa maendeleo ya soka nchini, kwa vigezo hivyo na ukizingatia leo tupo ktk sherehe ya Noeli, utalikubali ombi langu binafsi ntakalokuomba. Nimekaa nimetafakari sana, nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, nnafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari ameshatumikia karibia nusu ya kifungo chake, Ninajua kwa kufanya hivyo atakuwa kesha...

MAGAZETI YA LEO JUMANNE 27 DECEMBER 2016

Image

MAES AFUNGASHIWA VIRAGO KRC GENK

Image
Uongozi wa klabu ya KRC Genk hatiamaye umeamua kumtimua kazi kocha wake Peter Maes kwa kuwa na matokeo mabaya ambayo yalikuwa yakizidi kuporomoka.Taarifa kutoka kwenye mtandao wa klabu hiyo inaeleza kuwa chanzo ni kupata matokeo mabaya ndio mana wakaamua kusitishwa kwa ajira ya kocha huyo aliyejiunga na Genk msimu uliopita. Jupiler Rudi Cossey ambaye ni kocha msaidizi atabeba majukumu ya uongozi wa benchi la ufundi kwa muda huku wakiendelea kutafuta kocha mwingine.

ZLATAN IBRAHIMOVIC KUMSAFISHIA NJIA LINDELOF MANCHESTER UNITED

Image
MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic anaamini Msweden mwenzake, Victor Lindelof ana kipaji kung'ara katika timu kubwa duniani kufuatia kukua kwa tetesi za beki huyo wa Benfica kujiunga na Manchester United Januari. United imeingia kwenye mazungumzo na Rais wa Benfica, Luis Felipe Vieira juu ya uhamisho wa Pauni Milioni 38 Januari kwa ajili ya beki huyo wsa kati, ambaye amecheza mechi 11 za kimataifa. Na Ibrahimovic, ambaye alifikisha mabao 16 msimu huu baada ya kufunga mabao mawili mswishoni mwa wiki katika ushindi dhidi ya West Brom, amempigia debe mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. "Yeye (Lindelof) anakuwa. Ana majukumu mengi ya timu ya taifa sasa,"alisema Ibrahimovic. "Ni mzuri kiasi cha kutosha kwa United? Nafikiri yuko tayari kwa klabu kubwa nje ya huko. Ni juu yake anataka nini na mazingira yanasemaje. Chochote atakachochagua, itakuwa vizuri kwake.

Mwandishi wa habari ITV Arusha akamatwa na polisi

Image

MUANDISHI WA HABARI JIJINI ARUSHA ASWEKWA RUMANDE KWA AGIZO LA DC

Image
Mwandishi wa habari wa ITV mkoani Arusha Khalfan Lihundi anashikiliwa na polisi kituo cha Usa River wilayani Arumeru mkoani Arusha kwa tuhuma za kuandika habari za zinazodaiwa kuwa ni za uchochezi. Bw Lihundi amekamatwa jijini Arusha majira ya saa nane mchana na askari anayedaiwa kutumwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Bw Alexsander Mnyeti kama anavyoeleza Bw Basili Elias ambaye alishuhudia tukio hilo. Akizungumzia suala hilo mpiga picha wa Bw Khalifand Lihundi Bw Deogratius Kassamia amesema habari inayodaiwa kuwa ni ya uchochezi ilikuwa ni ya malalamiko ya wananchi juu ya tatizo la maji. Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha Bw Cloud Gwandu pamoja na kulaani kitendo hicho amesema hatua hiyo haikubaliki kwani haikufuata taratibu.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU MAITI 7 ZILIZOKUTWA MTO RUVU

Image
Jeshi la Polisi nchini limetoa ufafanuzi kuhusu miili 7 ya watu iliyokutwa ikielea katika mto Ruvu na kusema kuwa linaendelea na upelelezi kwa lengo la kuwatambua marehemu hao. Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Kamishna wa Polisi Robert Boaz, amesema jeshi hilo bado halijawatambua marehemu hao, huku akitetea uamuzi wa jeshi hilo kuzika haraka miili ya marehemu 6 kati ya 7. “Hatua zote za kitaalam zilifuatwa na tunaendelea kufanya upelelezi unaolenga kuwatambua marehemu hao na kujua ni jambo gani liliwasibu, tunawasihi wananchi kuendelea kutupa taarifa zitakazosaidia kutambulika kwa marehemu hao” Amesema Boaz Akielezea jinsi jeshi hilo lilivyopata taarifa, amesema jeshi hilo lilipata taarifa za kuelea kwa maiti 7 katika mto Ruvu eneo la Mkuruge wilayani Bagamoyo kati ya tarehe 6/12/2016 hadi 9/12/2016 ambapo askari na daktari walifika katika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa kitaalam. Amesema...

MAJAMBAZI YAUAWA JIJI MBEYA

Image
Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya wamefanikiwa kuzuia tukio la ujambazi katika mapambano ya kurushiana risasi na watu waliosadikiwa kuwa ni majambazi na kuua wawili kati yao. Taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari imesema kuwa mnamo tarehe 19.12.2016 majira ya saa 1:45 jioni katika Kijiji cha Busisya, Wilaya ya Rungwe, Askari Polisi walipata taarifa za siri za kuwepo kwa majambazi wenye silaha ambao walikuwa na lengo la kufanya uvamizi katika Duka la Mfanyabiashara wa soda na bia za jumla ambaye pia ni wakala wa kutuma na kupokea pesa kwa njia ya mtandao. Askari hao walianza kuwafuatilia majambazi hao na muda wa saa 1:45 jioni askari walikutana na majambazi hao wakiwa wamepakiana katika pikipiki ambapo baada ya majambazi hao kugundua kuwa wanafuatiliwa na askari walianza kuwarushia risasi askari na ndipo yalitokea majibizano ya risasi kati ya askari na majambazi hao. Askari walifanikiwa kuwapiga risasi majambazi wawili ambao walifariki ...

"SING'ATUKI NG'O" YAHYA JAMMEH

Image
Rais wa gambia Yahya Jammeh ameonya kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi wa kieneo kumlazimisha kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi na mfanyibiashara Adama Barrow. Akihutubia wanachama wa muungano wa Bar Afrika nchini humo Bw Jammeh alisema: ''Waje wajaribu kuniondoa.wanasubiri nini? mimi ni mtu mpenda amani lakini haimaanishi kwamba sitalitetea taifa langu, kwa ujasiri na uzalendo na kuibuka mshindi''. Amesema kuwa alikataa wito wa muungano wa viongozi wa mataifa ya Magharibi ECOWAS akiwemo rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia kuondoka nchini Gambia.Akiongezea: ''Wao ni kina nani wa kuniambia mimi niondoke nchini mwangu.Amewashtumu viongozi hao kwa kuingilia a ya ndani ya Gambia. ECOWAS tayari imesema kuwa inamtambua bw Barrow kama rais wa taifa hilo na kwamba litachukua hatua zozote kuhakikisha kuwa matokeo ya uchaguzi yanaheshimiwa.Viongozi wa kieneo watahudhuria kuapishwa kwa Bw Barrow mnamo mwez...

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI 22 DEC,2016

Image