MSHAMBULIAJI WA MBAO FC AFARIKI DUNIA AKIWA UWANJANI
Ismail Mrisho Khalfan akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuanguka uwanjani |
MSHAMBULIAJI wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Mbao FC ya Mwanza, Ismail Mrisho Khalfan amefariki dunia jana mjini Bukoba baada ya kuanguka uwanjani.
Mchezaji huyo alianguka Uwanja wa Kaitaba, Bukoba dakika chache baada ya kuifungia bao timu yae katika ushindi wa 2-0 kufuatia kugongana na mchezaji wa Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vijana Tanzania Bara.
Baada ya kuanguka alipatiwa huduma ya kwanza na kuonekana hali yake si ya kawaida, hivyo kukimbizwa hospitali ya mkoa wa Kagera kwa matibabu zaidi, ambako umauti ulimfika.
Mchezaji huyo amefariki akiwa ana umri wa miaka 19 na akiwa ametoka tu kufanya mtihani wa kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya Mwanza, maarufu 'Mwanza Seco'.
Comments
Post a Comment