WELBECK AANZA KUFANYA MAZOEZI
Baada ya miezi 7 ya kukaa nje ya kikosi kutokana na kupata maumivu ya kufundo cha mguu, hatimaye Welbeck ameanza kufanya mazoezi na kukimbia uwanjani.
Striker huyu wa England na Arsenal alipata tatizo msimu uliopita mwezi wa tano kwenye mechi dhidi ya Manchester City na mechi kuisha kwa suluhu.
Hijajulikana ni lini Danny atarudi kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal lakini inategemewa mwanzo mwa mwaka 2017 anaweza kurudi akiwa amepona kamili kabisa kwa ajili ya mechi za Arsenal.
Mwezi wa 10 manager Wenger alisema Welbeck yupo mbele zaidi ya mategemeo yao ya kupona kutokana na muda waliokadiria. Arsenal hawataki kumleta haraka mchezaji huyo uwanjani ili apone kamili kabisa.
Danny alijiunga na Arsenal akitokea Manchester united mwaka 2014 akitoka Manchester united.
Comments
Post a Comment