ZLATAN IBRAHIMOVIC KUMSAFISHIA NJIA LINDELOF MANCHESTER UNITED


MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic anaamini Msweden mwenzake, Victor Lindelof ana kipaji kung'ara katika timu kubwa duniani kufuatia kukua kwa tetesi za beki huyo wa Benfica kujiunga na Manchester United Januari.

United imeingia kwenye mazungumzo na Rais wa Benfica, Luis Felipe Vieira juu ya uhamisho wa Pauni Milioni 38 Januari kwa ajili ya beki huyo wsa kati, ambaye amecheza mechi 11 za kimataifa.

Na Ibrahimovic, ambaye alifikisha mabao 16 msimu huu baada ya kufunga mabao mawili mswishoni mwa wiki katika ushindi dhidi ya West Brom, amempigia debe mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.

"Yeye (Lindelof) anakuwa. Ana majukumu mengi ya timu ya taifa sasa,"alisema Ibrahimovic. "Ni mzuri kiasi cha kutosha kwa United? Nafikiri yuko tayari kwa klabu kubwa nje ya huko. Ni juu yake anataka nini na mazingira yanasemaje. Chochote atakachochagua, itakuwa vizuri kwake.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU