AMOAH APATA SHAVU URUSI
Daniel Amoah watatu kutoka kuliaakifanya mazoezi ya pamoja na wenzake Azam FC |
Klabu ya Ligi Kuu Urussi, Spartak Moscow inaripotiwa kuweka mezani ofa ya kumnyakua mlinzi wa Azam, Daniel Amoah.
Kwa mujibu wa mtandao wa Ghana, GhanaSoccernet, Spartak wameonesha nia ya kumchukua Amoah kwa kutangaza dau.
Amoah, raia wa Ghana mwenye umri wa miaka 20 alisajiliwa mwanzoni mwa msimu huu akitokea Medeama.
Azam walivutiwa na Amoah, 20 baada ya kumuona katika mashindano ya Kombe la Shirikisho akiichezea Medeama.
Comments
Post a Comment