ARSENE WENGER AMPONDA CARL JENKISON

Kipigo cha Arsenal kutoka kwa Southamton katika mchezo Kombe la Ligi uliopigwa jumatano na Arsenal kufungwa goli 2-0 kimemuibua kocha Wenger na kumtolea maneno beki wake Carl Jenkison ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kumuumiza beki huyo.arsene-wenger-carl
Wenger alisema kiwango cha Jenkison kwa siku za karibuni kimekuwa kibaya na hata kuchangia Arsenal kupoteza mchezo wa Southampton ambao umeifanya Arsenal kutupwa nje ya mashindano ya Kombe la Ligi.
Alisema kuwa tatizo kubwa ambalo linamsumbua Jenkison ni kujiamini na kuna muda anajiamini lakini muda mwingine anapoteza uwezo huo na kinachofuatia ni kufanya makosa ambayo yanaigharimu timu yake.
“Kama akiwa katika wakati mgumu anapoteza uwezo wa kujiamini na ukiangalia ni Jenkison yuleyule ambaye ana uwezo wa kucheza huo mpira. Kuna mambo hajakamilika sababu Jenkison hajiamini,” alisema Wenger.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU