NIYONZIMA ATUPWA NJE KIKOSI CHAKWANZA YANGA SC

KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima hayumo kabisa katika kikosi cha Yanga kinachomenyana na JKU ya Zanzibar katika mchezo wa kirafiki.

Tokeo la picha la niyonzima harunaKocha Mzambia, George Lwandamina amepanga kikosi chake cha kwanza Yanga leo kwa ajili ya mchezo na timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi na Niyonzima hayumo kabisa kwa sababu ni mgonjwa.

Lwandamina aliyechukua nafasi ya Mholanzi, Hans van der Pluijm ambaye sasa anakuwa Mkurugenzi wa Ufundi, amewapanga; Ally Mustafa 'Barthez', Hassan Kessy, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Nadir Haroub 'Cannavaro', Said Juma, Juma Mahadhi, Matheo Antony, Obrey Chirwa, Malimi Busungu na Geoffrey Mwashuiya.

Katika benchi Lwandamina aliyeanza kazi Yanga wiki mbili zilizopita amewaweka Deogratius Munishi 'Dida', Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Andrew Vincent 'Dante', Simon Msuva, Vincent Bossou, Thabani Kamusoko, Justin Zulu, Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Deus Kaseke na Kelvin Yondani.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU