MORINHO ATAKA NEYMAR ASAJILIWE MANCHESTER UNITED
Kutoka kwenye ripoti ya Daily Record ni kwamba kocha wa United ameweka macho kwa Neymar ambae anaonekana anataka sana kutoka nje ya Hispania sasa hivi.
Vilabu vya England vimepewa taarifa kuhusu matakwa ya Neymar licha ya kuwa na mkataba na Barcelona. Mourihno anajua kwamba anahitaji kuongeza moto kwenye safu yake ya ushambuliaji ili waweze kupata magoli mengi zaidi.
Inaaminika kwamba Manchester inatakiwa kulipa zaidi ya pound 180 millioni ili waweze kumtoa mchezaji huyo ndani ya Nou Camp.
Moja ya sababu zinazomfanya Neymar kutaka kuondoka Barcelona ni lengo lake la kutaka kuwa mchezaji bora duniani. Lakini sasa hivi akiwa ndai ya Barcelona anaonekana kufunikiwa na kivuli cha Messi. Kitu hicho kinamzuia kuwa nyota namba moja wa club hiyo.
Comments
Post a Comment