RONALDO AFANYA MAKUBWA HISPANIA
Mchezaji bora wa Dunia 2016, Christian Ronaldo ameiongoza klabu yake Real Madrid kutinga fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia inayofanyika nchini Japana, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2- 0 dhidi ya CF America.
Mfaransa Karim Benzima aliipatia Madrid bao la kwanza dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza, kabla ya mchezaji bora wa Dunia kwa sasa Christian Ronaldo kuipatia bao la pili na kuihakikishia klabu hiyo kucheza mchezo wa fainali.
Mchezo wa fainali utachezwa Disemba 18 katika uwanja wa Nissan uliopo Yokohama Japan ukiwakutanisha Real Madrid dhidi ya wenyeji Kashima Antlers saa 13:30 kwa saa za Afrika Mashariki.
Kashima Antlers mabingwa wa Ligi Kuu ya Japaa wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuvito vilabu vya Auckland City (2-1) hatua ya mtoaano, Mamelodi Sundowns (2-0) hatua ya robo fainali, Atletico Nacioal (3-0) hatua ya nusu fainali, huku Madrid wakianzia hatua ya nusu fainali kwa kuichapa CF America 2-0.
Comments
Post a Comment