MBUZI WAONJA RADHA NA UTAMU WA SODA
Na Hussein Mkuwia.
Wakulima wa zao la korosho mkoani mtwara wametoa kituko cha mwaka naweza kusema hivyo baada ya kuwanywesha soda na juisi mbuzi wao.
Kituko hicho ni muendelezo wa matukio hayo ya kustaajabisha jamii yaliyowahi kutokea siku zilizopita ni pamoja na mkulima mmoja (jina limehifadhiwa) kumpiga mkewe na kumuambia kuwa atampeleka kupata matibabu nje ya nchi, "Nina pesa nyingi sana na cjuwi nazitumia vipi ndio maana nimeamua nikuumize ili hizi pesa nizitumie katika matibabu yako" alisema mkulima huyo kumueleza mke wake.
Wakulima hao wanafanya hayo baada ya kuuza zao la korosho mnadani kwa bei nzuri ambapo waliuza Shilingi 3718 kwa kila kilo moja na kusema kuwa haijahi kutokea mkulima wa zao la korosho kuuza kwa bei ya juu kama ilivyo kwa utawala wa awamu ya tano.
Hivyo wakulima hao wamempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa kutengeneza mfumo mzuri wa uuzwaji wa mazao ya mkulima hasa mazao ya biashara na kufanya mkulima kuondokana na lindi la umaskini na kuheshimika katika jamii kama ilivyo kwa wafanyakazi wa serikalini.
Wakulima wa zao la korosho mkoani mtwara wametoa kituko cha mwaka naweza kusema hivyo baada ya kuwanywesha soda na juisi mbuzi wao.
Wakulima hao wanafanya hayo baada ya kuuza zao la korosho mnadani kwa bei nzuri ambapo waliuza Shilingi 3718 kwa kila kilo moja na kusema kuwa haijahi kutokea mkulima wa zao la korosho kuuza kwa bei ya juu kama ilivyo kwa utawala wa awamu ya tano.
Hivyo wakulima hao wamempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa kutengeneza mfumo mzuri wa uuzwaji wa mazao ya mkulima hasa mazao ya biashara na kufanya mkulima kuondokana na lindi la umaskini na kuheshimika katika jamii kama ilivyo kwa wafanyakazi wa serikalini.
Comments
Post a Comment