NGASSA ADONDOKEA MBEYA CITY FC

Sasa imedhihirika!! Baada ya tetesi ya takribani siku nne mfululizo, kiungo mshambuliaji wa pembeni Mrisho Ngassa sasa ni rasmi mali ya Mbeya City.

Ngassa ameonekana kwenye picha pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Mbeya City FC Dismas Ten wakiwa wameshika mikono ikiwa ni ishara ya kumkaribisha nyota huyo wa zamani wa Yanga klabuni hapo.

Safari ya Ngassa kutua Mbeya City imekuja baada ya kuachana na klabu ya Free State Stars FC ya Afrika Kusini na Fanja ya Oman.

Bado haijawekwa wazi ni mkataba wa muda gani ambao Ngassa amesaini na Wagonga Nyundo hao wa jiji la Mbeya.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU