MUANDISHI WA HABARI JIJINI ARUSHA ASWEKWA RUMANDE KWA AGIZO LA DC

Tokeo la picha la KHALFAN LIHUNDI

Mwandishi wa habari wa ITV mkoani Arusha Khalfan Lihundi anashikiliwa na polisi kituo cha Usa River wilayani Arumeru mkoani Arusha kwa tuhuma za kuandika habari za zinazodaiwa kuwa ni za uchochezi.

Bw Lihundi amekamatwa jijini Arusha majira ya saa nane mchana na askari anayedaiwa kutumwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Bw Alexsander Mnyeti kama anavyoeleza Bw Basili Elias ambaye alishuhudia tukio hilo.

Akizungumzia suala hilo mpiga picha wa Bw Khalifand Lihundi Bw Deogratius Kassamia amesema habari inayodaiwa kuwa ni ya uchochezi ilikuwa ni ya malalamiko ya wananchi juu ya tatizo la maji.

Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha Bw Cloud Gwandu pamoja na kulaani kitendo hicho amesema hatua hiyo haikubaliki kwani haikufuata taratibu.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU