SAMATTA APELEKA FURAHA KRC GENK


Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta usiku wa November 30 2016 ameingia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kuiongoza timu yake ya Genk kupata ushindi dhidi ya Waasland-Beveren.

Samatta akiwa na KRC Genk katika uwanja wa ugenini amefanikiwa kufunga magoli mawili katika ushindi wa goli 3-1, Samatta alifunga goli la kwanza dakika ya 15 goli la pili dakika ya 42 kabla ya mnigeria Wilfred Ndindikufunga goli la tatu dakika ya 80.

Wenyeji wa mchezo huo Waasland-Beveren walifanikiwa kupata goli la kufutia machozi dakika ya 89, kupitia kwa mchezaji wao Zinho Gano, huo ulikuwa ni mchezo wa Kombe la Croky.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU