MKWASA HAJAWASAHAU MBWANA SAMATTA,MOHAMED HUSSEIN NA KAPOMBE
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametaja kikosi chake bora cha kombaini ya Afrika Mashariki kwa mwaka 2016.
Katika kikosi chake, Mkwasa amemjumuisha beki wa pembeni wa Simba, Mohamed Hussein ambaye ameungana na mlinzi mwingine wa pembeni, Shomari Kapombe na Mbwana Samatta kutimiza idadi ya watanzania watatu katika chaguo la kikosi chake.
Mkwasa pia kamuorodhesha mshambuliaji mkongwe wa Uganda, Geoffrey Massa anayechezea klabu ya Baroka ya Afrika Kusini.
Katika mahojiano na mtando wa Blacknationtz blog, Mkwasa ameelezea kupendelea mfumo wa 4-2-3-1 ambao anadai unatoa uwiano mzuri wa kushambulia na kuzuia.
Comments
Post a Comment