KAMANDA WA POLISI MKOANI SINGIDA AFARIKI DUNIA

dsc_0145
Na Hussein Mkuwia

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Peter Kakamba amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mwili wa Marehemu utaagwa leo saa 11: 00 jioni katika hiyo na baadaye kusafirishwa kwenda Singida kwaajili ya kuagwa tena na baadaye kwenda nyumbani kwao Rukwa kwaajili ya mazishi.
Kamanda Kakamba alikuwa amelazwa hospitalini hapo akisumbuliwa na maradhi ya tumbo na alikuwa amefanyiwa oparesheni hivi karibuni.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU