HAJI MANARA AMUOMBEA MSAMAHA JERRY MURO KWA RAIS WA TFF
December 25 2016 mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Club ya Simba Haji Manara alitumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi kumuomba asamehewe afisa habari mwenzake wa Yanga Jerry Muro ambaye amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka.
Kwako Rais wa TFF
Kwanza nikutakie heri na baraka ktk sikukuu hii kubwa kabisa duniani kote. Nnakuandikia ujumbe huu mfupi na wa wazi
kwako, nikiamini wewe ni mtu mwelewa na mwenye huruma na upendo, pia ni kiongozi mwenye maono ya dhati kwa maendeleo ya soka nchini,

kwa vigezo hivyo na ukizingatia leo tupo ktk sherehe ya Noeli, utalikubali ombi langu binafsi ntakalokuomba.
Nimekaa nimetafakari sana, nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, nnafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari ameshatumikia karibia nusu ya kifungo chake,

Ninajua kwa kufanya hivyo atakuwa keshajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla,

HAJI MANARA
Comments
Post a Comment